Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) kuwa ligi ya tano kwa ubora barani Afrika na ya 39 duniani kwa mwaka 2022.
Kwa mujibu wa IFFHS, ligi 10 bora barani Afrika ni (kwenye mabano nafasi duniani);
- Misri (13)
- Algeria (20)
- Morocco (24)
- Sudan (33)
- Tanzania (39)
- Afrika Kusini (52)
- Angola (60)
- Tunisia (68)
- Nigeria (77)
- Zambia (79).