Kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers anaamini kikosi chake kimereja katika ubora baada ya kuitandika Aston Villa mabao manne kwa nunge, katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kwenye dimba la King Power.
Jamie Vardy alimaliza ukame wa magoli kwa kuifungia Leicester mabao mawili katika dakika ya 63 na 79, huku mabao mengine mawili yakifungwa na Harvey Barne katika dakika ya 40 na 85.
Ushindi huo unawafanya Leicester kuendelea kusalia katika nafasi ya tatu wakifikisha alama 53, wakati Aston Villa wakiwa katika nafasi ya 19 na alama zao 25 na sasa wana kazi ya ziada katika kujinasua na janga la kushuka daraja huku mchezo ujao wakikutana na Chelsea.
