Frank Lampard amepoteza mchezo wake wa kwanza aliporejea kwenye dimba la Stamford Bridge mbele ya timu yake ya zamani ya Chelsea akiwa kocha wa timu ya Derby Country kwenye michuano ya kombe la Ligi.
Magoli mawili ya kujifunga ya wachezaji wa Derby Country na goli moja lililotiwa kimiani na Cesc Fabregas yalitosha kabisa kuipa ushindi Chelsea wa bao tatu kwa mbili na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Magoli yote matano kwenye mchezo huo yalifungwa kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambao ulikuwa na kila aina ya mvuto hasa kwa mashabiki wa Chelsea ambao walimshangilia mno Frank Lampard ambaye aliichezea timu yao kwa miaka 13 kwa mafanikio makubwa.
Katika michezo mingine, Arsenal imesonga mbele baada ya kuilaza Blackpool bao mbili kwa moja,Tottenham Hotspurs imeiondosha West Ham United baada ya kuifunga bao tatu kwa moja na Middlesbrough ikaifunga Crystal Palace bao moja kwa bila.
Kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya kombe la Ligi, Arsenal itapambana na Tottenham, Chelsea itacheza na FC Bournemouth, Middlesbrough itakipiga na Burton Albion na Leicester au Southampton itapepetana na Manchester City au Fulham.