Lampard Afurahia Kurejea Stamford Bridge

0
200

Kocha wa timu ya Chelsea ya nchini England, – Frank Lampard amesema kuwa, ndoto yake imetimia baada ya kurejea tena kwenye uwanjawa Stamford Bridge akiwa kocha wa timu hiyo ingawa timu yake ilikosa ushindi kwenye mchezo wake wa kwanza katika dimba la nyumbani.

Chelsea ilitoka sare ya bao moja kwa moja na Leicester City pamoja na kutangulia kupata goli la mapema kupitia kwa kinda wa miaka Ishirini  Mason Mount  na wageni wakasawazisha kwenye dakika ya 67 kupitia kwa kiungo Mnigeria, –  Wilfred Ndidi.

Lampard anayeshikilia rekodi ya kuwa mchezaji alieifungia Chelsea magoli mengi,  amesema kuwa alijisikia faraja na ilikuwa siku muhimu  kwake kurejea tena Stamford Bridge,  sehemu ambayo alijizolea sifa nyingi enzi anacheza soka.

Kiungo huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya England anaamini kuwa,  kwake lilikuwa ni jambo kubwa kuingoza Chelsea kwenye dimba la Stamford Bridge pamoja na kwamba hawakushinda mchezo huo dhidi ya Leicester City.

Hadi sasa,Chelsea haijashinda mchezo wowote wa Ligi wakiwa na pointi moja baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Manchester United kwa bao Nne kwa bila na kuambulia sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Leicester City.