Kumsajili Ibrahimovic Spurs hakuna maana : Mourinho

0
957

Jose Mourinho amesema kumsajili Zlatan Ibrahimovic kwenye timu yake ya Tottenham Hotspur hakuna maana yoyote kwa sababu timu hiyo ina mshambuliaji bora kwenye ligi ya England ambaye  ni Harry Kane.

Ibrahimovic ambaye amewahi kuhudumu chini ya Mourinho wakati akiifundisha Inter Milan na Manchester United, kwa sasa hana timu na yupo huru kujiunga na timu yoyote.

Mourinho anasema yeye na Ibrahimovic ni zaidi ya marafiki na anakiri kuwa mshambuliaji huyo ni hatari,  lakini bado hana nafasi kwenye kikosi anachofundisha kwa sasa.

Mourinho amepewa kibarua cha kuinoa Spurs Jumatano iliyopita baada Mauricio Pochettino kufungashiwa virago,  na anasema hawawezi kusajili mshambuliaji mwingine wakati wana Harry Kane ambaye ni mshambuliaji hatari zaidi nchini England.

Kwa upande wake Harry Kane ambaye ameitumikia Spurs katika  michezo 269 na kufunga mabao 175 anasema kocha huyo ameshinda taji kwenye kila klabu aliyofundisha,  hivyo anaamini uwepo wake ndani ya Spurs utaondoa ukame wa mataji.