Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema kutokana na kuendelea kufanya vizuri, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi nane Afrika ambazo kombe la dunia litapita.
Mchengerwa amesema hayo leo mkoani Dar es Salaam na kueleza kwamba kombe hilo linatarajiwa kufika mwisho wa mwezi huu.
Katika hatua nyingine, amewatoa hofu mashabiki wa soka wanaotaka kwenda Afrika Kusini kuishangilia timu ya Simba SC katika mchezo wa raundi ya pili robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kuwa watakuwa salama.
“Niseme tu kwamba sisi kama Serikali tunafuatilia kwa karibu usalama wa timu na hivi ninavyoongea nimemteua msaidizi wangu Mkurugenzi wa Michezo ili aweze kuniwakilisha kusimamia hili,” amefafanua Mchengerwa.
Amesema Watanzania na Waafrika Kusini ni ndugu wa muda mrefu hivyo ni mategemeo kuwa hakutakuwa na jambo lolote linaloweza kuhatarisha usalama.