Kocha mpya wa Yanga atua Dar

0
123

Kocha Nasreddine Nabi raia wa Tunisia, ametua rasmi nchini hii leo, tayari kukinoa kikosi cha Yanga.

Kocha huyo ametua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es salaam majira ya saa 9 Alasiri, na kupokelewa na mmoja wa viongozi wa timu hiyo kutoka kampuni ya GSM, Mhandisi Hersi Said.

Akizungumza na Waandishi wa habari uwanjani hapo, Kocha Nasreddine Nabi amesema amekuja nchini kuinoa Yanga SC baada ya kuwepo kwa makubaliano kati yake na viongozi wa klabu hiyo,

Amesema amefurahi kupata nafasi ya kuifundisha Klabu hiyo ambayo ni kubwa Barani Afrika, yenye idadi kubwa ya Wachezaji wanaotambulika na pia yenye idadi kubwa ya mashabiki.