KMC kuwafuata Polisi Tanzania

0
161

Kikosi cha KMC FC kesho kitaondoka jijini Dar es salaam kuelekea jijini Arusha, kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania, mchezo utakaopigwa tarehe nne mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Msafara huo wa wana Kino Boys utakuwa na wachezaji 24, benchi la ufundi pamoja na viongozi.

KMC FC inakwenda jijini Arusha kusaka alama tatu muhimu ikiwa ugenini, na inakwenda ikiwa imejipanga kupata ushindi.

Kino Boys inahitaji ushindi kwenye mchezo huo, kwa kuwa katika duru ya kwanza ilipoteza mchezo dhidi ya Polisi Tanzania kwa kuifunga goli moja kwa sifuri katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

KMC FC pia itakutana na Coast Union tarehe saba mwezi huu katika uwanja wa Mkwawani jijini Tanga.