Kipchoge aweka rekodi Marathon

0
1043

Eliud Kipchoge amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za marathon, kukimbia Kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili.

Kipchoge ambaye ni Mwanariadha kutoka nchini Kenya, amekimbia Kilomita 42.2 katika muda wa saa Moja dakika 59 na Sekunde 40 katika shindano la Ineos mjini Vienna nchini Austria mapema hii leo.

Mwanariadha huyo ambaye ni Bingwa wa Olimpiki, alikuwa ameikosa rekodi hiyo kwa sekunde 25 katika jaribio lake la mwaka 2017.

Kipchoge ni bingwa mara Nne wa London Marathon.