Kim Paulsen aita 27 kuikabili Malawi

0
391

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Paulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini katikati ya mwezi ujao kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi kwa ajili ya kujianda na michezo ya hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Dunia.

Akitaja kikosi hicho Kocha Paulsen amesema kutakuwa na kambi mbili kabla ya kucheza mchezo wa awali wa kombe la Dunia ambapo mpaka sasa FIFA haijatoa ratiba ya michuano hiyo.

Kocha Paulsen amesema, kambi ya kwanza ya kikosi chake itaanza Juni 15, 2021 ambapo itakuwa maalum kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Malawi.

Kambi ya pili ya kikosi hicho itafanyika mwezi Agosti ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika katika majira ya joto mwaka 2022 nchini Qatar.

Kocha Paulsen amewaita katika kikosi hicho Magolikipa, Aishi Manula, Juma Kaseja na Metacha Mnata, walinzi wanaounda kikosi hicho ni pamoja na Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Mohamed Hussein, Edward Manyama, Erasto Nyoni, Bakari Mwamnyeto, Kennedy Juma, Nickson Kibabage na Dickson Job.

Viungo ni Simon Msuva, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Fesail Salum, Salum Abubakar, Byson Rafael, Iddy Nado.

Washambuliaji wa kikosi hicho ni Mbwana Samatta, John Bocco, Abdul Suleiman, Ayoub Lyanga, Dennis Kibu, Meshack Abrahamu, Novatus Dismas na Yussuf Mhilu.

Tanzania imepangwa Kundi J katika hatua hiyo ya mchujo pamoja na Madagascar, DR Congo na Benin.