Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Tanzania (Kilimanjaro Queens) inayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) , leo inashuka dimbani kucheza na timu ya Burundi katika michuano ya CECAFA ya Soka la Wanawake inayoendelea hapa nchini katika dimba la Azam Complex, Chamazi mkoani Dar es salaam.
Huo utakuwa mchezo wake wa Pili, baada ya kufungua michuano hiyo kwa kuitandika timu ya Sudan Kusini magoli Tisa kwa bila na sasa itakutana na Burundi iliyoanza kwa ushindi mnono wa magoli Matano kwa bila kwa kuitandika timu ya Zanzibar ya Wanawake (Zanzibar Queens).
Zanzibar Queens baada ya kupoteza mchezo wa kwanza, sasa itashuka dimbani kucheza na Sudan Kusini.
