Katika matokeo ya mchezo, Manchester United imekubali kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Crystal Palace wakiwa nyumbani kwenye dimba la Old Trafford.
Palace walianza kuwashtua Manchester United kwenye dakika ya 31 baada ya Jordan Ayew kufunga bao la kuongoza, kabla Daniel James hajaisawazishia Manchester United katika dakika ya 89 kisha Crystal Palace ikipata bao la ushindi katika dakika ya 91.