Kesi uchaguzi wa TFF yaunguruma Mahakama Kuu

0
343

Na Emmanuel Samwel

Upande wa madai umeiomba Mahakama Kuu ya Dar es Salaam kusitishwa kwa shughuli zote zinazohusiana na Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania mpaka pale kesi ya msingi namba 98 ya Mwaka 2021 itakaposikilizwa.

Ombi hilo limewasilishwa mawakili wa mdai ambaye ni Ally Salehe mbele ya Jaji Edwin Kakolaki leo.

Kesi hiyo namba 98 ya Mwaka 2021 iliyofunguliwa katika mahakama hiyo na Ally Salehe dhidi ya TFF na Bodi ya Wadhamini kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa TFF, imeahirishwa hadi saa 6 mchana leo kwa ajili ya uamuzi.

Hapo jana Mhakama Kuu ilitoa wito kwa Rais wa TFF, Wallace Karia, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Bodi ya Wadhamini ya TFF kufika mahakamani hapo kujibu hoja ya kwanini uchaguzi wa rais TFF usisimamishwe.