Japan imepata ushindi wa kushangaza ambao umeweka historia nchini hiyo ikiwafunga mabingwa wa kombe la Dunia mara nne, Ujerumani kwa mara ya kwanza katika historia ya soka.
Japan imefanikiwa kupindua meza katika Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa na kuondoka na alama zote tatu baada ya kuiadhibu Ujerumani 2-1.
Kufungwa kwa Ujerumani ni mwendelezo wa mshangao kwa timu zisizopewa nafasi kubwa kuwafunga wakongwe, ambapo jana Saudi Arabia iliifunga Argentina 2-1.