Jahazi la Warriors lazamishwa

0
865

Hali inazidi kuwa tete kwa Golden State Warriors baada ya kukubali kipigo cha alama 120 kwa 92 kutoka kwa Oklahoma City Thunder katika Ligi Kuu ya kulipwa ya mpira wa kikapu nchini marekani (NBA).

Denis Shiroda amefunga alama 22 na kucheza mipira iliyorudi yaani Rebounds Nane huku Danilo Galinari akifunga alama nyingine 21 na kulizamisha jahazi la Warriors waliokuwa wakiongozwa na Stephen Curry aliyefunga alama 23 na kucheza Rebounds Nane.

Huo ni mchezo wa Pili mfululizo kwa Warriors kupoteza tangu kuanza kwa msimu huu wa NBA na wabashiri wa mambo tayari wanaiona Warriors kama timu iliyopoteza makali yake kiasi cha kuiondoa kwenye mbio za ubingwa wa NBA.

Katika matokeo mengine Brooklyn Nets wamenyukwa alama 134 kwa 133 na Memphis Grizzlies wakati Portland Trail Blazers wakipata ushindi wa alama 121 kwa 119 dhidi ya Dallas Mavericks, huku Miami Heat wakishindwa kutamba mbele ya Minnesota Timberwolves na kunyukwa alama 116 kwa 109.