Harnaaz Sandhu kutoka India ameshinda taji la Miss Universe 2021, shindano lililofanyika katika mji wa Eilat kusini mwa Israeli.
Takribani warembo 80 kutoka sehemu mbalimbali duniani walijitokeza kuwania taji la Miss Universe 2021, huku michujo ikipunguza idadi ya washiriki na hatimaye kumpata mshindi ambaye ni Harnaaz.
Harnaaz mwenye umri wa miaka 21 ni mwanamitindo kutoka nchini India na taji la urembo la India na pia ni mwanamke wa tatu wa Kihindi kushinda taji la Miss Universe.
Nadia Ferreira wa Paraguay amekuwa mshindi namba moja na Lalela Mswane wa Afrika Kusini amekuwa mshindi namba tatu.
Shindano la Miss Universe 2021 lilishereheshwa na mchekeshaji Steve Harvey.