HESABU: Liverpool kutwaa ubingwa mapema Machi 21

0
521

Zikiwa imebaki michezo 13 Ligi Kuu ya England kumalizikia, mashabiki wengi wa soka wanaamini kuwa Liverpool itatwaa ubingwa mwaka kuu kutokana na kuwa katika kiwango cha juu. Licha ya kuwa wengi wanaamini klabu hiyo ndiyo mabingwa, lakini huenda hawajui ni lini itatwaa ubingwa huo.

Liverpool tayari imeweka kibindoni alama 73 baada ya kucheza michezo 25 ya ligi na kushinda michezo 23 huku ikienda sare/suluhu mchezo mmoja ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja.

Endapo itaendelea na kasi hiyo ya ushindi, itahitaji michezo sita, ambayo ni sawa na alama 18 ili kutangazwa kuwa mabingwa wa England kwa msimu wa 2019/20, kwani itafikisha jumla ya alama 91 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu nyingine yoyote hata zikishinda michezo yote 13 iliyosalia.

Kwa hesabu hizo Liverpool huenda wakatawazwa kuwa mabingwa wapya Machi 21 mwaka huu katika dimba lao la nyumbani, Anfield, wakatapoikaribisha Crystal Palace.

Hadi sasa Manchester United ndiyo inashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa mapema zaidi ambapo mwaka 2001 ilitwaa ubingwa Aprili 14 ikiwa na michezo 5 mkononi. Endapo Liverpool watafanikisha mbio zao, watavunja rekodi ya Man United, wakiwa na michezo 7 mkononi.

Aidha, kadri timu zinazoifuata Liverpool (Manchester City na Leicester City) zitakavyopoteza michezo, ndivyo zitakavyokuwa zinawapa vinara hao wa ligi nafasi ya kutwaa ubingwa kabla ya Machi 21.

Kutokana na kasi yake ya ushindi, Liverpool inatazamiwa kuvunja rekodi iliyowekwa na Man City mwaka 2018 kwa kuwa na jumla ya alama 100 baada ya michezo yote, ambapo kama Liverpool itashinda michezo yote 13 iliyobaki itakuwa imejikusanyia jumla ya alama 112.

Ratiba ya michezo ya Liverpool iliyosalia ni kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

TareheMichezo
Feb 15Norwich vs Liverpool
Feb 24Liverpool vs West Ham
Feb 29Watford vs Liverpool
Mar 7Liverpool vs Bournemouth
Mar 14Everton vs Liverpool
Mar 21Liverpool vs Crystal Palace
Apr 4Man City vs Liverpool
Apr 11Liverpool vs Aston Villa
Apr 18Brighton vs Liverpool
Apr 25Liverpool vs Burnley
May 2Arsenal vs Liverpool
May 9Liverpool vs Chelsea
May 17Newcastle vs Liverpool