Geita Gold FC na Singida Big Star zimetoshana nguvu katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kutoka sare ya goli 1-1.
Geita Gold ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika ya 9 ya mchezo likifungwa na mfungaji bora wa msimu uliopita, George mpole, kabla ya Mbrazil Rodrigo Fegu kusawazisha dakika mbili kabla ya mapumziko.
Kutokana na kila timu kuondoka na alama moja, Singida Big Star inakuwa nafasi ya tano ikiwa na alama 8 baada ya kushuka dimbani mara nne.
Kwa upande wa Geita Gold ipo nafasi ya 12 ikiwa na alama 3 baada ya kushuka dimbani mara nne.
Baada ya michezo ya leo, Ligi Kuu ya NBC itakwenda mapumziko kupisha ratiba ya FIFA ya michezo ya kimataifa.