Fury amchimba mkwara Wilder

0
490

Bondia Tyson Fury amesema anahitaji kumtwanga kwa knockout Deontay Wilder katika pambano lao la tarehe 22 mwezi huu jijini Las Vegas nchini Marekani, ili kuepuka maamuzi yenye utata kutoka kwa majaji kama ilivyokuwa katika pambano lao la kwanza.

Mwingereza huyo licha ya kumtandika Wilder mara mbili, bado anaamini alishinda katika pambano lao la mwisho liliochezwa mwezi Disemba mwaka 2018 licha ya majaji kuamua kuwa walitoka sare.

Furry anasema anaamini alimpiga Wilder, lakini ili kujihakikishia ushindi usio na ukakasi katika pambano linalokuja ni lazima amtwange kwa knockout kwani hataki tena maamuzi yenye utata kutoka kwa majaji.

Katika pambano lao la mwisho mjini Los Angeles, majaji walitoa ushindi wa alama 115-111 kwa Wilder, 114-112 kwa Fury na mmoja akatoa sare 113-113 kwa wote na pambano hilo kumalizika kwa sare na wengi wanasubiri kuona mambo yatakuwaje hiyo tarehe 22.