Floyd Mayweather anajitolea kugharamia mazishi ya George Floyd

0
780

Bingwa wa masumbwi Duniani Floyd Mayweather amesema anajitolea kugharamia mazishi ya George Floyd ambaye aliuawa na polisi wa Minneapolis

Maandamano ya kupinga mauaji ya George Floyd yamesambaa katika miji mbalimbali nchini Marekani na duniani kwa ujumla kulaani kitendo cha afisa polisi, Derek Chauvin kumkandamiza shingoni Floyd na kumsababishia kifo chake.

Habari kutoka Marekani zinasema,familia ya Floyd imekubali ofa ya Mayweather kugharamia mazishi ya ndugu yao.