FIFA yataka utaratibu wa kuandaa AFCON ubadilishwe

0
527

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) amewasihi viongozi wa soka Afrika kubadili mfumo wa uandaaji wa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zichezwe kila baada ya miaka minne badala ya utaratibu wa sasa ambapo huchezwa kila baada ya miaka miwili.

Gianni Infantino amesema endapo mashindano hayo makubwa zaidi ya soka Afrika yatafanyika kila baada ya miaka minne yatavutia watu wengi zaidi duniani kutazama.

Endapo pendekezo hilo litatekelezwa litavinufaisha pia vilabu mbalimbali vya soka barani Ulaya ambavyo huwa kwenye wakati mgumu kutokana na baadhi ya wachezaji wake wa kutegemewa kwenda kutumikia timu za taifa wakati michezo ya ligi ikiendelea.

Fainali zijazo zinatarajiwa kufanyika kuanzia Januari 9 hadi Februari 6, 2021 nchini Cameroon zikijumuisha timu 24 ambazo zitapangwa katika makundi sita.