FIFA yamweka kikaangoni Martinez

0
145

Shirikisho la soka Duniani (FIFA ) limefungua kesi dhidi ya timu ya Taifa ya soka ya Argentina kufuatia mlinda mlango wa timu hiyo Emiliano Martinez kuonesha ‘tabia ya kukera’ baada ya ushindi katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa nchini Qatar mwezi Desemba 2022.

Baraza la FIFA linalosimamia michezo limeanzisha uchunguzi baada ya ishara kadhaa za Martinez ambazo zimetafsiriwa kuwa ni chafu akiwa na tuzo ya golikipa Bora wa mashindano (Golden Glove).

Taarifa iliyotolewa na FIFA imesema kesi hiyo inahusu ukiukwaji wa kifungu cha 11 (tabia ya kukera na ukiukaji wa kanuni za uchezaji wa haki) na kifungu cha 12 (utovu wa nidhamu wa wachezaji na viongozi).

Itakumbukwa, ishara yake ya kutwaa taji la Golden Glove kabla ya Kombe la Dunia kukabidhiwa ilienea kwa kasi, na aliendelea kumkejeli Kylian Mbappe wa Paris Saint-Germain katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo, na pia wakati wa gwaride baada ya kurejea nyumbani kwao Argentina.

Credit : Simulizinasauti