FIFA yaiondolea Kitayosce zuio la kusajili

0
200

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeiondolea klabu ya Kitayosce adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji.

FIFA imechukua hatua hiyo baada ya klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC kulipa madai ya kocha Ahmed Soliman ambaye amewahi kuifundisha klabu hiyo.

Raia huyo wa Misri aliishitaki Kitayosce FIFA kwa kuvunja mkataba kinyume cha taratibu.

Kwa hatua hiyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nalo limeiondolea Kitayosce adhabu ya kufungiwa kusajili.