Federer na Nadal watesa

0
525

Bingwa wa zamani katika mchezo wa Tenisi,  Roger Federer na mshindi wa mataji 11 ya mchezo huo Rafael Nadal,  wametinga katika hatua ya tatu ya mashindano ya wazi ya Ufaransa bila kupoteza seti hata moja.

Bingwa wa mwaka 2009 Roger Federer ambaye anacheza mashindano ya wazi ya Ufaransa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015, alihitaji saa moja na dakika 36 kumsukuma nje ya michuano hiyo Mjerumani, Oscar Otte kwa seti tatu kwa bila za ushindi wa 6-4, 6-3 na 6-4.

Kwa upande wake bingwa mtetezi wa michunao hiyo Mhispania,- Rafael Nadal amepata ushindi wa seti tatu kwa bila za ushindi wa 6-1, 6-2 na 6-4 dhidi ya Mjerumani, – Yannick Maden.

Kwa akina dada Johanna Konta amekuwa Muingereza wa kwanza tangu mwaka 1992 kutinga hatua ya tatu ya mashindano ya wazi ya Ufaransa tangu alipofanya hivyo Lauren Davis.

Konta ambaye ametoka kuugua, amemshinda Lauren wa Marekani kwa seti mbili kwa moja za ushindi wa 6-3 1-6 na  6-3 na sasa atakutana na Viktoria Kuzmova wa Slovakia katika hatua ya tatu ya mashindano hayo hapo kesho.