Fainali ni Yanga na USM Alger

0
574

Yanga SC itaikaribisha USM Alger ya Nigeria katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, mkoani Dar es Salaam Mei 28 mwaka huu.

Juni 3 shughuli itahamia nchini Algeria ambapo Yanga itakuwa mwenyeji wa USM Alger katika mchezo wa pili wa fainali ambapo mshindi wa jumla wa michezo yote miwili ndiye atakuwa bingwa.

Yanga imeandika historia Afrika ikitinga fainali hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya magoli 4-1.

Aidha, USM Alger imetinga fainali baada ya kuitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa jumla ya magoli 2-0, ushindi ambao imeupata katika uwanja wa nyumbani baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa suluhu.

Rais wa Tanzania, ameipongeza Yanga kwa kutinga hatua hiyo akisema “Mmeandika historia na kuipa nchi yetu heshima kubwa sana. Nawatakia kila la kheri katika mchezo wenu wa Fainali.”