Msimu mpya wa ligi ya kulipwa ya mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA) unaanza alfajiri ya Oktoba 17 mwaka huu kwa kupigwa michezo miwili, ambapo bingwa mtetezi Golden State Warriors watamenyana na Oklahoma City Thunder.
Thunder wanaingia kwenye mchezo huo bila huduma ya nyota wake Russell Westbrook ambaye anauguza jeraha la goti alilofanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
Inakadiriwa kuwa nyota huyo atakuwa nje kwa wiki nne kuuguza jeraha lake ambapo kocha wa Oklahoma City Thunder, – Billy Donovan amekiri kuwa mwanzo wa msimu utakuwa mgumu bila ya nyota wake huyo.
Warriors wao wanaingia kwenye msimu mpya wakiwa na morali baada ya kikosi chake kutokuwa na majeruhi huku pia ikiwa ndio bingwa mtetezi wa ligi hiyo.
Wapenzi wa ligi ya kulipwa ya mpira wa kikapu nchini Marekani wanasubiri kuona ni nini atafanya nyota wa mchezo huo Lebron James akiwa na timu yake mpya ya Los Angeles Lakers baada ya kufanya vyema kwenye timu aliyotoka ya Cleveland Caveliers.
Mchezo mwingine utakaopigwa alfajiri ya kesho Oktoba 17 unawakutanisha Boston Celtics wanaowakaribisha Philadelphia 76ERS kwenye dimba la TD Garden mjini Boston,- Miami.