Dube ajitia kitanzi Azam FC

0
183

Azam FC imengia mkataba mpya wa miaka miwili zaidi na mshambuliaji wake wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube.

Mkataba huo utamfanya Dube kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2024.

Dube ambaye amesajiliwa msimu huu, amekuwa na kiwango bora ambapo hadi sasa ndiye kinara wa magoli kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) akiwa na mabao 14.

Mbali na mabao hayo 14, kiujumla msimu huu, Dube amefunga mabao 17 kwenye mashindano yote, mengine matatu akitupia katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).