Drake awekewa ngumu Milwaukee

0
379

Vyombo vya habari zikiwemo Redio katika mji wa Milwaukee nchini Marekani vimeendelea kutekeleza ahadi yao ya kutocheza wimbo wowote wa msanii Drake,  mpaka fainali za Ligi ya Kulipwa ya mpira wa Kikapu ya nchini humo NBA zitakapomalizika.

Imeelezwa kuwa sababu kubwa ya marufuku hiyo ni kutokana na tabia ya msanii huyo kutoka Toronto nchini Canada kuwa msumbufu hasa kwa wachezaji pindi anapoenda kuangalia mechi za NBA.

Katika fainali ya NBA kwa Kanda ya Mashariki,  timu ya Toronto Raptors anayoshabikia Drake imemenyana na timu ya Milwaukee Bucks na Drake amekuwa akipewa upendeleo wa kukaa hadi kwenye benchi la ufundi na wakati mwingine kuongea na wachezaji huku ikielezwa kuwa amekuwa akigombana na wachezaji wa timu pinzani.

Katika kutekeleza marufuku hiyo baadhi ya radio katika mji wa Milwaukee ziliondoa kabisa nyimbo za Drake katika orodha ya vipindi mbalimbali ikiwemo Top Ten na Play List za vipindi mbalimbali na hazikupigwa kabisa wakati wa michezo miwili ya kwanza ambayo Milwaukee walishinda yote,  japo alfajiri ya kuamkia hii leo wamepoteza mchezo wa kwanza kwao.