Dodoma Jiji yagawana dhahabu na Geita Gold

0
334

Mchezo kati ya Dodoma Jiji FC dhidi ya matajiri wa dhahabu Geita Gold umemalizika kwa kushuhudia sare ya kufungana bao 1-1 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Geita Gold walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Daniel Lyanga dakika ya 78 ya mchezo, na Waziri Junior akasawazisha mwishoni katika dakika nne za nyongeza za mchezo.

Kwa matokeo hayo Dodoma Jiji inafikisha alama 17 na Geita Gold wanafikisha alama 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.