Klabu ya Yanga imefanya mabadiliko na kutangaza kamati mpya ya mashindano ya klabu hiyo.
Kamati hiyo itafanya kazi za usimamizi wa mashindano ambayo kikosi cha Yanga kinashiriki msimu ujao,Imekuwa ni siku chache uongozi wa klabu hiyo kuzitenganisha kamati mbili zilizokuwa zinafanyakazi pamoja ya usajili na mashindano iliyokuwa chini ya mwenyekiti wake, Franky Kamugisha.
Walioteuliwa katika kamati hiyo ni Mwenyekiti, Rodgers Gambo na makamu wake ni Saad Khimji. Katibu wa kamati ni Edwin Mshagama na wajumbe ni Hamad Islam, Yanga Makaga, Ally Kamtande, Leonard Bugomola, Said Side, Bunnah Kamoli, Soud Mlinda, Martin Mwampashi, Hamza Jabir, Edward Urio, Kawina Konde, Abednego Ainea na Tom Lukuvi.