Kuelekea mpambano wa watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba siku ya Jumapili, Mfanyabiashara maarufu nchini Azim Dewji ameahidi kutoa tiketi mia tatu kwa mashabiki watakaojitokeza siku ya Ijumaa na Jumamosi katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) iliyopo jijini Dar es salaam kuchangia damu, ili kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali mbalimbali.
Dewji ametoa ahadi hiyo ikiwa zimesalia siku 2 kabla ya kufanyika kwa mtanange huo kati ya Yanga na Simba katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.