Danjuma atua Tottenham kwa mkopo

0
179

Klabu ya soka ya Tottenham Hotspurs ya England imemsajili kwa mkopo Arnaut Danjuma kutoka Villarreal hadi mwisho wa msimu wa mwaka 2022/23.

Danjuma ambaye ni Mzaliwa wa Nigeria alianzia maisha yake ya soka nchini Uholanzi akiwa na TOP Oss na PSV kabla ya kujiunga NEC Nijmegen mwaka 2016.

Baada ya kufunga magoli 14 katika mechi 46 za wakubwa katika misimu miwili akiwa na NEC, alijiunga na Club Brugge ya Ubelgiji kisha akazichezea AFC Bournemouth na Villarreal.

Katika ngazi ya kimataifa ameifungia timu ya Uholanzi magoli mawili katika michezo sita aliyovaa jezi ya Taifa lake.