Coastal Union yaiadhibu Kagera Sugar 2-0

0
499

Coastal Union FC ya mkoani Tanga imepanda hadi nafasi ya 9 ya msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuichapa Kagera Sugar FC magoli 2-0 katika Uwanja wa Mkwakwani.

Magoli ya Wagosi wa Kaya yamefungwa na Moubarack Hamza dakika ya 10 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 65.

Kufuatia kipigo hicho, Kagera Sugar ipo nafasi ya 15 ikiwa na alama mbili baada ya kushuka dimbani mara tatu ambapo imetoka sare michezo miwili na kupoteza mitatu.