Timu ya Manchester City imefufua matumaini ya mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya England, baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao Manne kwa Moja dhidi ya Burnely.
Mabao ya Man City yamefungwa na Gabriel Jesus aliyefunga mabao mawili, mabao mengine yamefungwa na Rodrigo Hernández Cascante na Riyad Mahrez.
Kwa matokeo hayo, City imefikisha alama 32 nyuma ya mahasimu wao wanaowania ubingwa huo Liverpool, ambayo ina alama 40.
Matokeo ya mchezo mwingine, Crystal Palace imebuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya AFC Bournemouth, bao lililofungwa na Jeffrey Schlupp.
Ligi Kuu hiyo ya England inaendelea hii leo kwa michezo kadhaa kuchezwa, huku mchezo wa kuvutia zaidi utakuwa ni wa Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspur utakaochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford ambao kocha mpya wa Spurs, – José Mourinho anarejea ndani ya uwanja huo ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu atimuliwe kuinoa United.