Christian Eriksen ala shavu Inter Milan

0
562

Klabu ya Inter Milan imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa Tottenham Hotspur, Christian Eriksen kwa ada ya uhamisho takribani Tsh bilioni 50.8.

Eriksen mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Inter Milan kwa mkataba wa miaka minne na nusu

Baada ya kuitumikia Tottenham kwa miaka saba, katika kipindi cha joto nyota huyo aliwaambia waajiri wake hao kwamba anataka changamoto mpya mwishoni mwa msimu uliopita.

Baada ya nia yake ya kwenda Hispania msimu uliopita kushindikana, alianza msimu na Tottenham ambapo hadi anaondoka amecheza michezo 28 msimu huu.

Kwa sasa Inter Milan ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Serie A ikiwa alama tatu nyuma ya vinara wa ligi ambao ni Juventus.