Hazard afikiria kuondoka Stamford Bridge

0
558

Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, -Eden Hazard amesema kuwa anafikiri mchezo wa fainali ya michuano ya Yuropa dhidi ya Arsenal ndiyo mchezo wake wa mwisho kuitumikia klabu hiyo.

Hazard aliyehudumu Stamford Bridge kwa muda wa miaka saba  amesema kuwa,   anadhani ni wakati wa kusema kwaheri kwa matajiri hao wa London ingawa amesema chochote kinaweza kutokea kwa sababu anasubiri waajiri wake wamruhusu.

Miamba ya soka Barani Ulaya, – Real Madrid inasemekana tayari wamefikia makubaliano na nyota huyo raia wa Ubelgiji,  na kinachosubiriwa ni baraka pamoja na makubaliano ya dau la uhamisho kutoka Chelsea.

Hazard ameitumikia Chelsea katika  michezo 352,  na kuifungia mabao 110 na anasema ndoto yake ilikuwa kucheza Ligi Kuu ya England na hilo tayari limetimia,  hivyo ni wakati muafaka wa  kutafuta changamoto mpya.