Chelsea wachezea kipigo darajani, mashabiki walia na VAR

0
368

Daraja la Chelsea the blues limevunjika vipande viwili baada ya kutandikwa mabao mawili kwa bila dhidi ya Manchester United na kunyimwa mabao mawili dhidi ya mfumo wa maamuzi uwanjani kwa msaada wa video (VAR)

Mabao ya Manchester United yamefungwa na Martial dakika ya 45 kabla ya mapumziko huku bao la pili likifungwa na Harry Maguire dakika ya 66

VAR ikitoa maamuzi kuhusu goli la Giroud

Kwa matokeo hayo Chelsea wanaendelea kubaki nafasi ya nne wakiwa na alama 41 huku Manchester united ikisogea hadi nafasi ya 7 wakikusanya jumla ya alama 38 baada ya michezo 26