CAF YATANGAZA WAAMUZI WA SUDAN KUAMUA HATMA YA AZAM NA WAETHIOPIA

0
243

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limechagua waamuzi kutoka nchini Sudan kuchezesha nchezo wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Azam FC na Fasil Kenema ya Ethiopia.

Mchezo huo wa kwanza wa Azam FC unatarajiwa kuchezwa  Uwanja wa Taifa wa Bahir, Agosti 11 mwaka huu mjini Bahir, Ethiopia majira ya saa 10:00 jioni.

Mwamuzi wa kati wa mchezo huo, anatarajia kuwa Elsiddig Mohamed Eltreefe, mwamuzi msaidizi namba moja akiwa, Elmoiz Ali Mohamed Ahmed na namba mbili akisimama Haitham Elnour Ahmed huku Sabri Mohamed Fadul akiwa mwamuzi wa akiba.

Kamishna atayesimamia mchezo huo anatarajia kutokea kwenye visiwa vya Reunion, ambaye ni Ismael Locate.