Bongo Muvi kufanya kazi na wizara ya Afya

0
141

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Molell leo Juni 29 amekutana na kundi la wasanii la Taasisi ya MAMA ONGEA NA MWANAO linaloongozwa na Steven Mengele maarufu kama ‘Steve Nyerere’ jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, wamekubaliana namna ya kufanya kazi kwa pamoja na wizara hiyo kwa lengo la kutumia kazi yao ya sanaa kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu masuala ya afya nchini.

Dkt. Mollel amesema wasanii ni kioo cha jamiii hivyo wamekubali kufanya nao kazi katika kuhakikisha kwamba Watanzania wote nchini wanafikiwa na taarifa muhimu zihusuyo masuala ya afya.

Kwa upande wake Steve Nyerere amesema wamefurahi kukutana na viongozi hao ambao wamekubaliana masuala mbalimbali yakiwemo utoaji wa vifaa tiba kwa wananchi na kutoa jumbe mbalimbali zinazohusiana na masuala ya afya nchini.