Bondia Mtanzania amtwanga Mjerumani kwa TKO

0
162

Bondia Mtanzania anayeishi nchini Sweden Awadhi Tamim amemtwanga bondia Shkelqim Ademaj wa Ujerumani kwa TKO katika pambano la raundi 10 lililofanyika Essen nchini Ujerumani.

Awadh ameshinda taji lililokuwa wazi la WBF ambapo mpinzani wake alishindwa kuendelea na pambano hilo.

Awadhi alianza kwa kumlambisha sakafu Ademaj katika raundi ya sita lakini baadae aliamka na kuruhusiwa kuendelea na pambano.

Aliongoza kwa pointi wakati wote wa pambano hilo hadi lilipovunjwa kutokana na Ademaj kushindwa kuendelea.

Hivi Karibuni bondia huyo wa Tanzania anayeishi nchini Sweden alikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango alipokuwa ziarani nchini humo ambapo alimueleza juhudi zake katika kuitangaza Tanzania kupitia mchezo huo wa masumbwi pia alimuahidi kuliwakilisha vema Taifa katika pambano hilo la uzito wa juu lililofanyika Ujerumani.