Bodi ya Ligi yabadili muda wa kuanza mechi ya Yanga na Azam

0
168

Bodi ya ligi -TPLB imefanya mabadiliko ya muda wa kuanza kwa Mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Na. 251 kati ya Yanga na Azam fc ulipangwa Saa moja usiku siku ya Jumapili April 25, mwaka huu na sasa utachezwa saa 2:15 usiku siku hiyo hiyo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

TPLB imesema Sababu ya mabadiliko hayo ni uwanja huo kuwa na matumizi mengine mchana.