Bashungwa ataka michezo ya wenye ulemavu kupewa Kipaumbele

0
242

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amewaagiza watendaji wote wa sekta ya michezo kuhakikisha michezo ya wenye ulemavu, hususani soka kuwa miongoni mwa michezo ya kipaumbele na kuitaka kuingizwa kwenye mifumo rasmi ya kukuza vipaji, kama UMITASHUMTA na UMISSETA.

Bashungwa ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua mashindano ya Afrika ya Mpira wa Miguu kwa watu Wenye ulemavu kwa Wanaume (CANAF 2021) katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

“Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambua thamani na fursa zilizopo katika michezo yote, ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu. Kwa msingi huo tumechukua jukumu hili, ili kuhakikisha fursa hii inatumika vema kuiweka timu yetu ya soka ya Taifa kwa walemavu (Tembo Warriora) katika ramani ya mchezo huu kimataifa,” smefafanua Bashunga

Mkurugenzi wa Michezo nchini ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya michezo hiyo hapa nchini, Yusufu Omary Singo amesema serikali itaendelea kusimamia michezo yote kikamilifu ikiwa ni pamoja na michezo ya wenye ulemavu.