Barcelona yatupwa nje Europa League

0
172

Ushindi wa jumla wa magoli 4-3 umeiwezesha Manchester United kusonga mbele hatika hatua ya robo fainali ya Europa League.

United imepata ushindi wa magoli 2-1 katika mchezo wa marudiano, na hivyo kuwatupa nje ya mashindano Barcelona baada ya mchezo wa kwanza timu hizo kumaliza kwa sare ya magoli 2-2.

Katika mchezo huo, Barcelona ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli lililofungwa na Robert Lewandowski kwa mkwaju wa penati, kabla ya Fred kusawazisha na kisha Antony kufunga goli la ushindi.

Huu ni ushindi wa kwanza wa Man United dhidi ya Barcelona tangu mwaka 2008 waliposhinda 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kwa msimu wa pili mfululizo Barcelona inatolewa kwenye mashindano ya Ulaya katika hatua za mapema.