Barcelona yarejea kileleni

0
1234

Timu ya Barcelona ya nchini Hispanua imerejea kileleni kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza nchini humo maarufu kama La Liga baada ya kuishushia kipigo cha mabao matano kwa bila timu ya Levante.

Mchezaji Lionel Messi alionekana kuwa mwiba mchungu kwa Levante akihusika kwenye mabao yote matano, akafunga mabao matatu yaani Hat Trick na kutoa pasi za mabao yaani assist mbili kwa wachezaji Luis Suarez na Gerad Pique.

Katika matokeo mengine ya michezo ya ligi ya La liga iliyochezwa Jumapili Disemba 16, timu ya Sevilla nayo imepanda hadi nafasi ya pili baada ya kuifunga timu ya Girona mabao mawili kwa bila.

Espanyol wamenyukwa nyumbani mabao matatu kwa moja na Real Betis huku Huesca wakitoka sare ya mabao mawili kwa mawili na Vila Real.

Kwa matokeo hayo, timu ya Barcelona sasa wana alama 34 wakifuatiwa na Sevilla wenye alama 31 sawa na Atletico Madrid waliopo kwenye nafasi ya tatu na alama 31, pia wakitofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na nafasi ya nne ikiwa ni ya Real Madrid wenye alama 29.