Barbara: Simba vs Kaizer Cheifs ni mechi ngumu

0
383

Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba SC, Barbara Gonzalez amesema kuwa mchezo wao wa mzunguko wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ni mchezo mgumu.

Gonzalez amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amewataka Watanzania na mashabiki wengine wa Simba kuiombea dua timu yao ili ishinde mchezo huo.

“Hii mechi ni ngumu sana. Bado tunahitaji dua na sala zenu ili tusogee tunapostahili Insha’Alla,” ameeandika Gonzalez.

Mchezo huo utapigwa leo saa 1:00 jioni (saa za Afrika Mashariki) katika dimba FNB jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Katika mchezo wa kwanza wa robo fainali uliopigwa Mei 14, 2021 nchini Algeria, wageni Wydad AC ya Morroco ilifanikiwa kuwavuta shati wenyeji wao MC Alger kwa kutoka sare (1-1).