AZAMA FC YAENDELEZA MCHAKA MCHAKA WA KIMATAIFA

0
241

KIKOSI cha Azam FC kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea kwenye mchezo wao kimataifa wa kombe la Shirikisho dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia.

Azam FC ambao ni mabingwa wa kombe la Shirikisho, watamenyana na Fasil Kenema, Agosti 10 ikiwa ni mchezo wa awali kabla ya kurudiana nao uwanja wa Chamazi, Dar.

Ofisa Habari wa Azam FC, Japhary Idd Maganga amesema kuwa mchakamchaka unaendelea ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.

“Utakuwa mchezo mgumu na mkubwa kwetu hivyo tunajipanga ili kuona namna gani tunaipeperusha Bendera ya Taifa kimataifa zaidi,” amesema.

Azam FC walitwaa ubingwa huo baada ya kushinda mbele ya Lipuli FC kwa bao 1-0 lililopachikwa na Obrey Chirwa.