Klabu ya Azam imetangaza kufikia makubaliano ya pande mbili na kocha Abdihamid Moallin na msaidizi wake Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi.
Taarifa ya klabu hiyo imesema makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni hapo katika nafasi nyingine ambazo zitatangazwa hapo baadaye.
Kwa sasa timu ya Azam itakuwa chini ya Daniel Cadena ambaye ni kocha wa makipa, hadi atakapotangazwa kocha mpya.
Cadena ni kocha mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha, UEFA Pro License.