Azam walambwa Kilimanjaro

0
953

Ligi kuu soka Tanzania Bara imeendelea leo katika viwanja mbalimbali huku kila timu ikiendelea kujiimarisha ili kufanya vizuri katika ligi hiyo yenye msisimko mkubwa msimu huu

Huko Jijini Tanga kutoka uwanja wa Mkwakwani Wagosi wa Kaya Coastal Union imelazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya wageni KMC FC ya Kinondoni mkoani Dar es salaam

Mechi ya pili imepigwa katika dimba la Ushirika mkoani Kilimanjaro mchezo ukimalizika kwa Azam fc kulazwa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Polisi Tanzania

Mchezo wa baadae utapigwa kutoka Uwanja wa Mkapa Dar es salaam majira ya Saa 1 jioni utawakutanisha Wana Jangwani Dar es salaam Young African wakicheza na Geita Gold Fc mchezo
utakaorushwa moja kwa moja kupitia TBC TAIFA