Azam FC yatinga fainali Mapinduzi Cup

0
284

Azam FC imetinga fainali ya Mapinduzi Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 9-8 dhidi ya Mabingwa watetezi Yanga katika mchezo nusu fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Timu hizo zimefika hatua ya penati baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana.

Yanga ilikuwa bingwa mtetezi wa kombe hilo ililolitwaa mwaka jana baada ya kuifunga Simba SC katika mchezo wa fainali.

Azam inasubiri mshindi katika ya Simba SC na Namungo, mchezo ambao utapigwa majira ya saa 2:15 usiku.

Usikose kufuatilia mchezo huo kupitia TBC Taifa na TBCOnline.