Aryna aitaka fainali dhidi ya Azarenka

0
168

Aryna Sabalenka anasema anatamani kucheza fainali ya michuano ya wazi ya Australia mwaka huu na raia mwenzake wa Belarusi Victoria Azarenka, ili kuweka historia katika michuano hiyo na taifa lao.

Azarenka ambaye ni bingwa mara mbili wa michuano hiyo anacheza na bingwa wa Wimbledon, Elena Rybakina katika nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo leo Alhamisi.

Sabalenka anayeshika nafasi ya tano katika viwango vya ubora kwa wanawake, atachuana na Magda Linette wa Poland katika nafasi ya pili.

Imekuwa ni bahati kwao kushiriki michuano hiyo, kwani wanamichezo wa Belarus wamepigwa marufuku na mashirika kadhaa ya usimamizi wa michezo kwa sababu ya nchi hiyo kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.